Shalom Redio imefunguliwa chini ya kanisa la Kaloleni Pentecoste, na kusimamiwa na uongozi wa kanisa. Kazi kubwa na lengo kuu la Shalom Redio ni kuutangaza ufalme wa Mungu kwa mataifa na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, ili kulitimiza agizo kuu la Kristo, Marko 16:15-16.